Yanga kurejesha heshima mbele ya CFFA?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Yanga kurejesha heshima mbele ya CFFA?

Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga, Jumamosi hii ya Oktoba 17 wanashuka dimbani kuvaana na CFFA ya Madagascar katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL).

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, saa 9:00 alasiri, ukiwa na umuhimu wa kipekee kwa pande zote mbili zinazowania nafasi hiyo adhimu barani Afrika.

Yanga ina faida ya nyumbani

Licha ya CFFA kuwa wenyeji wa mchezo huu wa kwanza, wawakilishi hao wa Madagascar walilazimika kuchagua Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kama uwanja wao wa nyumbani baada ya kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya CAF katika nchi yao.

Hali hii inawapa Yanga faida kubwa ya kisaikolojia na kimazingira, kwani watacheza mechi zote mbili bila kusafiri nje ya nchi, huku wakizungukwa na maelfu ya mashabiki wao.

Yanga itaingia katika mchezo huu ikitoka kupoteza dabi ya Kariakoo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, kwa mabao 2-1 mnamo Oktoba 10. Machungu hayo ya ligi ya ndani yanatarajiwa kuwa chachu kwa kikosi cha Wananchi kupambana kwa nguvu zote ili kupata ushindi mnono utakaoweka mguu mmoja ndani ya hatua ya makundi na kurejesha tabasamu kwa mashabiki wao.

CFFA si timu ya kubeza

Kwa upande wao, mabingwa wa Madagascar, CFFA FC, wamewasili wakiwa na dhamira ya kuonyesha kuwa hawakufika hatua hii kwa bahati mbaya. Baada ya kuiondoa Lijabatho FC ya Lesotho kwa jumla ya mabao 3-1 katika raundi ya kwanza.

CFFA ni timu inayocheza kwa nidhamu kubwa ya kujilinda na kutumia mashambulizi ya kushtukiza mbinu ambayo wanatarajia kuitumia kwenye mchezo huo.

Akizungumza baada ya timu hiyo kuwasili nchini juzi, kocha wa timu hiyo Franck Rajaonarisamba alijinasibu kuifahamu vyema Yanga akiwataja baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao walikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Tanzania iliyocheza mechi ya kuwania kufuzu Afcon 2027 dhidi ya Madagascar na mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 nchini Morocco.

Beki wa kulia wa timu hiyo Radoniaina Rabemanantsoa alicheza dakika zote 90 za mchezo huo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
36m ago
READ MORE β†’
Manara ajiweka kitanzini Yanga
Manara ajiweka kitanzini Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Mwenda anarejea, kumuongezea Yao nguvu upande wa kulia
Mwenda anarejea, kumuongezea Yao nguvu upande wa kulia
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 15 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 15 2026
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA
20h ago
READ MORE β†’
Job ni suala la muda kikosini Yanga
Job ni suala la muda kikosini Yanga
1d ago
READ MORE β†’
CFFA tayari wameshawasili Dar
CFFA tayari wameshawasili Dar
1d ago
READ MORE β†’
Vingilio; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Vingilio; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 14 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 14 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’