Manara ajiweka kitanzini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Manara ajiweka kitanzini Yanga

Aliyekuwa msemaji wa Yanga Haji Manara amejiweka katika nyakati ngumu Kufuatia mzozo ulioibuka kati yake na Msemaji wa sasa wa Yanga Ali Kamwe na kauli zake za ukusoaji uongozi wa Yanga pamoja na kushiriki mijadala iliyoandaliwa na waajiri wake wa zamani Simba.

Hatua hiyo imeweka rehani hatma ya uanachama wake Yanga huku taarifa za ndani zikidokeza kuwa ameondolewa kwenye baadhi ya makundi ya Wanayanga kwenye mitandao ya kijamii.

Shinikizo la kutaka anyang’anywe uanachama linazidi kuongezeka kufuatia kile kinachotajwa na baadhi ya viongozi na wanachama kama mfululizo wa kauli na vitendo vinavyokiuka maadili, kulinda nembo, na heshima ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.

Aidha, katika kile kinachoonekana kama tamko lisilo rasmi lakini lenye uzito mkubwa kutoka ndani ya uongozi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Alex Ngai, ametumia ukurasa wake wa Instagram kurusha "jiwe kizani" lililomlenga moja kwa moja Manara.

Katika chapisho hilo, Ngai aliandika: "Sisi hatujawahi kukimbia kwetu tupo na tutafia Kwetu. Foreigners mliokimbilia kwetu rudini kwenu kumesha tengamaa. Nimeshindwa kushikilia bomba," aliandika Ngai

Mzozo huu umeshika kasi baada ya dabi ya Kariakoo ya mnamo Oktoba 10, 2026, ambapo Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC. Baada ya mchezo huo, Manara alijitokeza hadharani na kuipongeza Simba kwa kiwango bora, akisisitiza kuwa walistahili ushindi huo kutokana na maandalizi na mbinu zao uwanjani.

Manara pia alipingana waziwazi kauli zilizoibuliwa mitandaoni na kupewa uzito na msemaji wa Yanga Ali Kamwe zikidai kuwa wachezaji wa Simba walitumia 'sindano' au dawa za kusisimua misuli kupata ushindi.

Manara alizikemea kauli hiyo na kuziita ni visingizio vya "kijinga" vinavyolenga kuficha makosa ya kiufundi ya timu.

Kusifu upinzani na ushirikiano na Ahmed Ally

Jambo jingine linalotajwa kuwakasirisha Wanayanga ni mfululizo wa machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii, hasa baada ya Simba kuifunga Mashujaa FC mabao 6-1, ambapo Manara alisifu mfumo wa 'pressing' wa Simba na kuonya kuwa wanaweza kutwaa mataji yote msimu huu kama Yanga haitabadilika.

Pia, kitendo chake cha kufanya mahojiano ya pamoja na Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, kilitafsiriwa na mashabiki wenye msimamo mkali kama usaliti wa wazi na ishara ya "kurudi nyumbani" kufuatia historia yake ya nyuma na wekundu hao wa Msimbazi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
CFFA wanaandaliwa dozi ya kuwatosha
35m ago
READ MORE β†’
Yanga kurejesha heshima mbele ya CFFA?
Yanga kurejesha heshima mbele ya CFFA?
3h ago
READ MORE β†’
Mwenda anarejea, kumuongezea Yao nguvu upande wa kulia
Mwenda anarejea, kumuongezea Yao nguvu upande wa kulia
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 15 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 15 2026
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA
20h ago
READ MORE β†’
Job ni suala la muda kikosini Yanga
Job ni suala la muda kikosini Yanga
1d ago
READ MORE β†’
CFFA tayari wameshawasili Dar
CFFA tayari wameshawasili Dar
1d ago
READ MORE β†’
Vingilio; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Vingilio; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 14 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 14 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’