Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Aziz Ki kurejea mechi dhidi ya CFFA

Baada ya kukosa mchezo wa ligi kuu  dhidi ya Simba akitumikia adhabu ya kadi nyekundu, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki anatarajiwa kurejea kikosini mwishoni mwa wiki wakati Yanga itakapomenyana na CFFA ya Madagascar kwenye mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya Mabingwa (CAFCL)

Kurejea kwa Aziz Ki ni habari njema kwa kocha Manqoba Mngqithi kwani anatarajiwa kuongeza ubunifu katika safu ya ushambuliaji.

Yanga inahitaji kushinda mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Azam Complex ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi pale timu hizo zitakaporudiana siku nne baadae kwenye uwanja huohuo.

CFFA iliwasili nchini jana ambapo leo kikosi hicho kimeanza maandalizi tayari kuwakabili mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Upande wa Yanga, kikosi kiliingia kambini baada ya mchezo dhidi ya TRA United kusogezwa mbele, Wananchi wakipata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa.

Hata hivyo wakati Aziz Ki akirejea, Yanga imepata pigo wakitarajiwa kumkosa kiungo kiraka Duke Abuya aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema Abuya anaweza kukosekana kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Job ni suala la muda kikosini Yanga
Job ni suala la muda kikosini Yanga
8h ago
READ MORE β†’
CFFA tayari wameshawasili Dar
CFFA tayari wameshawasili Dar
9h ago
READ MORE β†’
Vingilio; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Vingilio; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 14 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 14 2026
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mwenda arejeshwa rasmi kikosini Yanga
Mwenda arejeshwa rasmi kikosini Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Abuya nje wiki mbili
Abuya nje wiki mbili
1d ago
READ MORE β†’
Malengo yetu mbio za ubingwa Ligi Kuu yako palepale - Kamwe
Malengo yetu mbio za ubingwa Ligi Kuu yako palepale - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa
1d ago
READ MORE β†’
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
1d ago
READ MORE β†’