Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda

Kiungo na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda, Khalid Aucho, ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa baada ya kuitumikia nchi yake kwa miaka 13, akihitimisha safari iliyoambatana na mafanikio na kumbukumbu muhimu katika historia ya The Cranes.

Aucho ametangaza uamuzi huo kupitia taarifa rasmi aliyoitoa Oktoba 12, 2026, akieleza kuwa amejivunia kuvaa jezi ya taifa lake tangu alipoanza kuitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza Novemba 30, 2013.

Katika kipindi chake cha kuitumikia Uganda, kiungo huyo amecheza mechi 77 za kimataifa na kufikia hatua ya kupewa jukumu la unahodha, akiwa sehemu ya kizazi kilichoiwakilisha nchi hiyo katika mashindano makubwa ya soka barani Afrika.

Miongoni mwa mafanikio aliyoyataja ni kushiriki katika safari ya Uganda kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), baada ya kusubiri kwa miaka 38 bila kufanikiwa kufikia hatua hiyo. Pia ameiwakilisha nchi yake katika matoleo matatu ya mashindano hayo.

Aucho amesema ndoto yake ya utotoni ilikuwa kuisikia timu ya taifa ikiimba wimbo wa taifa kwenye majukwaa makubwa ya soka duniani, akieleza kuwa kufikia hatua ya kucheza na baadaye kuiongoza timu hiyo kama nahodha ni heshima kubwa katika maisha yake.

Akikumbuka safari yake, kiungo huyo ameeleza kuwa alikulia katika mazingira ya kawaida, akifanya kazi katika machinjio ya soko la Bugembe, lakini alikuwa na matarajio makubwa ya siku moja kuichezea nchi yake katika kiwango cha juu cha soka.

Katika taarifa hiyo, Aucho ametoa shukrani kwa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), viongozi wa soka, makocha waliomsaidia katika safari yake, pamoja na wachezaji wenzake ambao ameshirikiana nao katika nyakati mbalimbali za mafanikio na changamoto.

Amewataja makocha waliokuwa sehemu ya safari yake akiwamo Milutin “Micho” Sredojevi, Sébastien Desabre, Johnathan McKinstry na Paul Put, huku akitoa heshima maalumu kwa marehemu Fred Kajoba, ambaye amesema mchango na imani yake vilikuwa na athari kubwa katika maisha yake.

Aidha, amewashukuru mashabiki wa Uganda kwa sapoti yao, akieleza kuwa hamasa yao katika Uwanja wa Namboole na maeneo mbalimbali nchini iliendelea kuwaongezea nguvu wachezaji wa timu ya taifa walipokutana na changamoto.

Licha ya kuhitimisha safari yake ndani ya timu ya taifa kama mchezaji, Aucho amesema dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono maendeleo ya soka la Uganda haijabadilika. Ameeleza kuwa sasa ni wakati wa kizazi kipya kujitokeza, kuvaa jezi ya taifa na kuandika historia yao wenyewe.

“Naondoka katika timu ya taifa nikiwa na moyo uliojaa shukrani, fahari kubwa na upendo usiopimika kwa nchi yangu,” amesema Aucho katika ujumbe wake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
2h ago
READ MORE β†’
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
3h ago
READ MORE β†’
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
7h ago
READ MORE β†’
Yanga itarejea ikiwa imara zaidi
Yanga itarejea ikiwa imara zaidi
21h ago
READ MORE β†’
Mabosi Yanga kufanya tathmini kipigo dhidi ya Simba
Mabosi Yanga kufanya tathmini kipigo dhidi ya Simba
1d ago
READ MORE β†’
Kuumia kwa Abuya kulitugharimu - Manqoba
Kuumia kwa Abuya kulitugharimu - Manqoba
1d ago
READ MORE β†’
Mchezo dhidi ya TRA United kupangiwa tarehe nyingine
Mchezo dhidi ya TRA United kupangiwa tarehe nyingine
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 2-1 Yanga, Ligi Kuu (FT)
Highlights; Simba 2-1 Yanga, Ligi Kuu (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 11 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 11 2026
1d ago
READ MORE β†’