Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi amesema majeraha aliyopata kiungo Duke Abuya yalichangia kwa kiasi kikubwa kikosi chake kupoteza mchezo wa ligi kuu dhdi ya Simba baada ya kuzidiwa eneo la kiungo.
Abuya alipata majeraha mwanzoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kufanyiwa madhambi na winga wa Simba Libasse Gueye.
Akizungumza baada ya mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-1, Manqoba alisema walipoteza umiliki eneo la kiungo baada ya Abuya kutoka.
"Ngoma ni mchezaji mzuri na alitusaidia, lakini nikiri Abuya ni mtu tofauti. Mpango wetu ulitetereka baada ya kuumia."
"Ni mchezaji anayepambana sana wakati wote akiwa tayari kujitoa kwa asilimia 100 na ana ubora mkubwa kwenye mapambano ya kuwania mpira," alisema Manqoba.
Aidha kocha huyo alitoa ufafanuzi mabadiliko ya kumtoa Mudathir akibainisha kuwa yalikuwa ni mabadiliko ya lazima kwa kuwa alichoka.
Kipigo hicho kimeishusha Yanga nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi huku watani zao Simba wakipanda kileleni baada ya kufikisha alama 21.