Simba walikuwa bora, Yanga wameonyesha uchovu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Oct 2026
Simba walikuwa bora, Yanga wameonyesha uchovu

Mengi yatasemwa lakini mwisho wa siku Wanayanga wanapaswa kukubali, Simba walikuwa bora sana kila idara wakionekana kuitaka mechi zaidi kuliko wachezaji wa Yanga.

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi anaweza kulaumiwa kwa sababu ni yeye aliyepanga wale wanaume 11 walioingia uwanjani kuipambania Yanga kwenye mchezo huo waliokubali kipigo cha mabao 2-1.

Lakini kwa tathmini ndogo tu unaweza kuona leo Yanga ilizidiwa sio kimbinu tu bali kwenye utimamu wa kimwili wa wachezaji.

Ukiangalia takwimu za mchezo huo zinakuonyesha Yanga hawakukimbia sana kama walivyofanya Simba. Kwa mara ya kwanza leo wamemiliki mchezo chini ya asilimia 40, hii ni mechi ya kwanza kwa Yanga kucheza chini ya kiwango kiasi hicho msimu huu.

Kwa dakika zote 90 za mchezo Yanga imepiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango huku Simba wakipiga mashuti 6 on target. Yanga ilitengeneza nafasi kubwa tatu tu wakati Simba walitengeneza nafasi 14.

Kipindi cha pili wachezaji wa Yanga walionekana kuwa wamechoka zaidi, wakilazimishwa kukaa nyuma kwa muda mwingi kwani hata mipira ilipopelekwa mbele haikukaa.

Ikumbukwe idadi kubwa ya wachezaji wa Yanga (10) walikuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa na wengine wamerejea siku mbili kabla ya mchezo huo.

Haiwezi kuwa sababu pekee iliyopelekea Yanga kupoteana lakini ni wazi baadhi yao walikuwa na uchovu na pengine ndio maana hawakutoa uwezo wao kwa asilimia 100.

Sio suala la Yanga kupoteza leo lakini ni wazi timu haikuwa katika kiwango bora cha ushindani, pengine hapa ndipo uongozi na benchi la ufundi wanapaswa kuanzia.

Yanga SC Stories

Bobosi katika rada za Yanga
Bobosi katika rada za Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatangaza viingilio mchezo dhidi ya MC Alger, CAFCL
Yanga yatangaza viingilio mchezo dhidi ya MC Alger, CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni MC Alger, Zanzibar
Kituo kinachofuata ni MC Alger, Zanzibar
20h ago
READ MORE β†’
Fadlu aweka mkakati hatua ya makundi CAFCL
Fadlu aweka mkakati hatua ya makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
1d ago
READ MORE β†’
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
1d ago
READ MORE β†’
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
1d ago
READ MORE β†’