Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi ameweka wazi kuwa muda waliopata wa kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba umekiweka katika chake katika nyakati nzuri kukabiliana na wapinzani wao wakuu.
Manqoba amesema amepata wiki mbili za kukiandaa kikosi chake, kuwasoma wapinzani wake kwa kina na kufahamu ubora na madhaifu yao hivyo kuelekea mchezo huo wa ligi kuu utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru, wanafahamu kile wanaenda kufanya.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mapema leo, Manqoba alisema wanazichukulia dakika 90 za mchezo huo kwa umuhimu mkubwa na anaamini wataondoka na furaha baada ya filimbi ya mwisho.
"Tumepata muda wa kutosha wa kujiandaa kwa ajili ya dabi, ambapo tumetumia takribani wiki mbili kufanya kila tuwezalo kuboresha mfumo wetu wa kiufundi."
"Tumeangalia nguvu na udhaifu wao, tukafanya uchambuzi wa kina wa mchezaji mmoja mmoja ambaye tunaona anaweza kutuletea madhara."
"Mpaka kufikia sasa, hakuna kingine zaidi kinachoweza kufanywa na mimi au benchi la ufundi, bali tunasubiri kuona kitakachotokea uwanjani katika mechi hiyo itakayokuwa ngumu na yenye ushindani mkubwa kwa pande zote mbili."
"Ninayo matumaini makubwa kwamba mwisho wa mchezo huo, sisi ndio tutakaokuwa upande unaosherekea ushindi," alisema