Wote waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa wamerejea - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Wote waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa wamerejea - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema maandalizi ya kikosi cha timu hiyo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba yanaendelea vyema.

Yanga imejichimbia kambini Avic Town kujiandaa na mtanange huo utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 10 kwenye uwanja wa Uhuru.

Kamwe amesema kwa sasa kikosi cha Yanga kimekamilika baada ya wachezaji wote waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa kuripoti kambini.

"Tunaendelea vyema na maandalizi yetu, tunafurahi wachezaji wote waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa wamerejea wakiwa wako fiti kabisa, hakuna yeyote aliyepata majeraha," alisema Kamwe.

Kamwe amewahakikishia wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa kikosi chao kitakuwa tayari kwa mapambano ya kuwania alama tatu kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Licha ya tambo za wapinzani wao, Kamwe amesema wao wamewekeza nguvu zaidi kwenye maandalizi yao na siku ya Jumamosi yule aliyejiandaa vizuri ataonekana pale uwanja wa Uhuru.

Tiketi zimeanza kuuzwa.

Katika hatua nyingine, Bodi ya ligi imethibitisha kuanza kwa mauzi ya tiketi kuelekea mtanange huo.

Tketi hizo zinapatikana kupitia mtandao rasmi wa tiketi wa TFF.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Safari hii hakuna mambo ya kufanya mazoezi ya mwisho
Safari hii hakuna mambo ya kufanya mazoezi ya mwisho
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 08 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 08 2026
7h ago
READ MORE β†’
Hizo hizo asilimia ndogo ndiyo Yanga inazozitaka
Hizo hizo asilimia ndogo ndiyo Yanga inazozitaka
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amuachia kazi maalum Zakouane Kariakoo Derby
Aziz Ki amuachia kazi maalum Zakouane Kariakoo Derby
21h ago
READ MORE β†’
Hivi hapa viingilio Dabi ya Kariakoo Jumamosi
Hivi hapa viingilio Dabi ya Kariakoo Jumamosi
1d ago
READ MORE β†’
Mwenda aamuliwa kurejea Yanga atumikie mkataba wake
Mwenda aamuliwa kurejea Yanga atumikie mkataba wake
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 07 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 07 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mwalimu afunga mawili, Tanzania U-23 yaaga AFCON
Mwalimu afunga mawili, Tanzania U-23 yaaga AFCON
1d ago
READ MORE β†’
Mabondia Mafia Boxing Promotion waitembelea Yanga Avic Town
Mabondia Mafia Boxing Promotion waitembelea Yanga Avic Town
1d ago
READ MORE β†’
Yanga, Safari Lager wazindua msimu wa tatu Safari Lager Cup
Yanga, Safari Lager wazindua msimu wa tatu Safari Lager Cup
1d ago
READ MORE β†’