Ambani 'awachana' Waarabu baada ya kutolewa mapema Urusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jun 2018
Ambani 'awachana' Waarabu baada ya kutolewa mapema Urusi
Morocco na Misri tayari zimeiaga michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko Urusi baada ya kupoteza michezo yao miwili mwanzo .

Misri ilichapwa na Uruguay/Urusi wakati Morocco ilichapwa na Irani/Ureno hivyo kuwa timu za kwanza kabisa kuyaaga mashindano hayo.

Boniface Ambani, mshambuliaji wa zamani wa Yanga aliyeisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi Kuu msimu wa 2008/09 yeye akiibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 18, hakushangazwa na timu hizo kutolewa mapema.

"Hawa watu acha wapigwe warudi Africa," ameandika Ambani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

"Mwaka mmoja (2009) tulienda Misri kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa. Tuliposhuka uwanja wa Ndege wakatukejeli kwa kutuuliza Afrika inaendeleaje?"

"Nikashangaa sana nakujiuliza kwani hapa tulipotua ni Ulaya au?"

"Vituko walivyotufanyia sasa! Wakatupeleka Hotel mbaya, tukagoma na kuwaambia tunataka hoteli ya nyota tano, ilichukua saa tano kutusikiliza."

"Vikafuata vituko vya uwanjani, wanapewa mabao hakuna! Mchezaji wao akiguswa eneo la hatari jua ni penati."

"Morocco, Tunisia na Misri ni vizuri tu watolewe warudi nyumbani mapema. Hawajui maana ya mchezo wa kiungwana."

"Mateso nliyopata mikononi mwa hawa watu ni Mungu pekee ndiye ajuae. Karibuni Afrika, nanyi mmeonjeshwa kile mnachotufanyia!"

Maneno ya Ambani yameungwa mkono na wadau wengi kwani sio siri Mataifa hayo yamekuwa na kawaidia ya kutengeneza mazingira magumu kwa timu wanazopambana nazo katika viwanja vyao vya nyumbani.

Tabia hiyo imekuwa ikiwasaidia kutawala soka la Afrika lakini wakitoka nje ya Afrika timu zao hufungwa kirahisi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’