Doumbia amepata chimbo jipya Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Doumbia amepata chimbo jipya Morocco

Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga, Mohamed Doumbia, amepata chimbo jipya la kazi akijiunga na klabu ya Hassania d’Agadir inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Morocco (Botola Pro).

Doumbia, raia wa Ivory Coast, alijiunga na miamba hiyo ya soka la Morocco kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima akitokea Yanga SC.

Hatua hii inakuja baada ya kiungo huyo kumaliza muda wake wa mkopo katika klabu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ambako alicheza kwa mafanikio makubwa msimu uliopita kabla ya kurejea kwa muda jijini Dar es Salaam kwa klabu yake ya Yanga.

Ripoti kutoka nchini Morocco zinaeleza kuwa Doumbia tayari amejumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Hassania d’Agadir na ameanza vyema majukumu yake.

Katika michezo yake miwili ya kwanza tangu asajiliwe, kiungo huyo amefanikiwa kucheza kwa dakika zote 90, jambo linalothibitisha kuwa tayari ameshateka imani ya benchi la ufundi la timu hiyo.

Huu ni msimu wa mwisho wa mkataba wake wa miaka miwili na Yanga, Doumbia atakuwa mchezaji huru mara baada ya mkataba wake wa mkopo nchini Morocco kumalizika.

Yanga SC Stories

BBD yuko tayari kuendeleza alipoishia
BBD yuko tayari kuendeleza alipoishia
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 04 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 04 2026
14h ago
READ MORE β†’
Yanga Princess mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
Yanga Princess mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yajipima na JKT Tanzania Gymkhana
Yanga yajipima na JKT Tanzania Gymkhana
1d ago
READ MORE β†’
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea
TFF yaruhusu wachezaji Yanga, Simba, Singida BS kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Yanga Princess kusaka mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
Yanga Princess kusaka mshindi wa tatu Ngao ya Jamii
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 03 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Badru afichua Kazimoto kupandishwa kikosi cha kwanza
Badru afichua Kazimoto kupandishwa kikosi cha kwanza
2d ago
READ MORE β†’
Chuga Boy aongezwa kikosi cha Stars U23
Chuga Boy aongezwa kikosi cha Stars U23
2d ago
READ MORE β†’
Dabi ya Kariakoo kupigwa dimba la Uhuru
Dabi ya Kariakoo kupigwa dimba la Uhuru
2d ago
READ MORE β†’