Kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Abushir 'Chuga Boy' amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania U23 inayojiandaa na mchezo wa marudiano kuwania kufuzu Afcon U23 dhidi ya Kenya.
Chuga Boy alikuwa kwenye kikosi cha Ngorongoro Heroes ambacho hivi karibuni kilishiriki michuano ya CECAFA U20 na kufanikiwa kutinga fainali ambayo walipoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya Sudan.
Licha ya kupoteza mchezo huo, Ngorongoro Heroes walifuzu michuano ya Afcon U20 wakiwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Sudan.
Chuga alipachika mabao mawili katika michuano hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Sasa anakwenda kuipambania U23 ambayo ilichapwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Kenya.