Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Pacome Zouzoua ameanza kutembea kawaida pasipo kutumia msaada wa magongo.
Hii ni hatua muhimu katika uponaji wa jeraha la kifundo cha mguu alilopata mwishoni mwa msimu uliopita.
Kwa takribani miezi minne mfululizo, Pacome ameendelea kupatiwa matibabu ili kuhakikisha anapona na kuweza kurejea katika majukumu yake.
Aina ya jeraha alilopata na hatimaye kuanza kutembea bila msaada wa magongo, ni jambo la kumshukuru Mungu na kuwapongeza madaktari wanaomhudumia pamoja na uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said ambaye aliahidi watatumia kila aina ya gharama ili kuhakikisha mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga anarejea uwanjanii


