Kikosi cha Yanga kilirejea mazoezini jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 10 jijini Dar es saalam.
Mkufunzi wa Yanga Manqoba Mngqithi anakiandaa kikosi chake ili kuhakikisha anapata ushindi wa pili kwenye Derby hiyo ya Kariakoo.
Tayari kocha huyo raia wa Afrika Kusini ana ushindi kwenye begi akiingoza Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii August 12.
Safari atawaongoza Wananchi kuwania alama tatu muhimu zitakazomuhakikishia kuendelea kukalia usukani wa ligi kuu ya NBC.

