Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ni miongoni mwa wachezaji waliorejea mazoezini kikamilifu baada ya mapumziko kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba.
Wananchi wamerejea kujiandaa na mtanange huo utakaopigwa Oktoba 10 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mzize na beki wa kati Dickson Job wote walikuwa sehemu ya wachezaji walioshiriki program za kwanza za mazoezi hapo jana.

Baada ya kupata nafasi ya kurejea kikosini kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold na kuonyesha kiwango kizuri, ni wazi Mzize yuko katika nafasi nzuri ya kuikabili Simba Oktoba 10.
Urejeo wake ni habari njema kwa kocha Manqoba Mngqithi kwani amemuongezea machaguo kwneye safu yake ya ushambuliaji kuelekea mtanange huo ambao Yanga imepania kuendeleza ubabe dhidi ya watani zao hao wa jadi.
Wakati wa mapumziko, Mzize alionekana akifanya mazoezi makali ufukweni kujiweka tayari ikiwa ni ishara kwamba sasa yuko fit sawasawa na tayari kukabidhiwa majukumu makubwa kwenye kikosi cha Yanga.