Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1d ago
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga

Familia ya aliyekuwa Mwanachama na shabiki maarufu wa Yanga SC, Haji Omari Ramadhani Mpili, imetoa shukrani kwa klabu ya Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said kwa namna walivyomhudumia marehemu wakati wa kipindi cha ugonjwa wake hadi alipofariki dunia.

Shukrani hizo zilitolewa jana na mwanaye wakati wa msiba wa Mzee Mpili uliofanyika Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

Mzee Mpili alifariki dunia usiku wa Jumapili, Septemba 27, 2026, katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri alipokuwa akipatiwa matibabu. Mazishi yake yalifanyika Jumatatu, Septemba 28, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Ikwiriri.

Katika msiba huo, viongozi mbalimbali wa Yanga walifika kutoa heshima za mwisho, akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai, Ofisa Mtendaji Mkuu Andre Mtine na Meneja wa Habari Ally Kamwe. Mamia ya wananchi pamoja na mashabiki wa klabu zote kubwa nchini walishiriki katika mazishi hayo.

Akizungumza baada ya mazishi, Ngai alisema Mzee Mpili alikuwa mwanachama aliyekuwa akiipigania Yanga kwa muda wote wa maisha yake.

Klabu hiyo pia ilitoa ubani wa Sh1.1 milioni, huku kundi la wanachama wa Black Card likikabidhi Sh3 milioni kwa familia ya marehemu.

Yanga SC Stories

Yanga Princess bado haijajipata
Yanga Princess bado haijajipata
25m ago
READ MORE β†’
Pacome sasa anatembea bila magongo
Pacome sasa anatembea bila magongo
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
6h ago
READ MORE β†’
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
9h ago
READ MORE β†’
Kangwanda anauwasha moto Zambia
Kangwanda anauwasha moto Zambia
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya Kariakoo Derby
Maandalizi ya Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
1d ago
READ MORE β†’
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
1d ago
READ MORE β†’
SPATA yaingilia kati sakata la Mwenda, Yanga
SPATA yaingilia kati sakata la Mwenda, Yanga
1d ago
READ MORE β†’