Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Ijumaa, itashuka uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kuikabili Guinea Bissau katika mchezo wa kuwania tiketii ya michuano ya Afcon 2027.
Kwa Tanzania huu ni mchezo ambao ni sehemu ya kipimo cha utayari kwa Stars kuelekea michuano hiyo ambayo Tanzania, Kenya na Uganda zimeandaa kwa pamoja.
Tayari timu hizo wenyeji zina tiketi mkonon lakini kwa mujibu wa kanuni za CAF, zitashiriki hatua ya makundi.
Nyota wa Yanga Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Mohamed Hussein, Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kocha Miguel Gamondi kitakachoshuka dimbani leo kuzisaka alama tatu katika mchezo wa kwanza.
ADVERTISE HERE