Ngoma ameanza taratibu, ni suala la muda tu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2026
Ngoma ameanza taratibu, ni suala la muda tu Yanga

Alipowasili Jangwani, uongozi wa Yanga uliweka wazi hitaji lake kubwa kupata kiungo mwenye uwezo wa kuimarisha eneo la ukabaji na usambazaji wa mpira, nafasi ambayo ilibaki na pengo tangu kuondoka kwa Mganda Khalid Aucho.

Katika dirisha la usajili lililopita, Wananchi walielekeza nguvu zao nchini Morocco na kumnasa Fredy Ngoma kutoka Olympic Safi, klabu ambayo msimu uliopita ilifanya vizuri hadi kufika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Ngoma alifika Yanga akiwa na jukumu kubwa la kuziba pengo hilo, lakini mwanzo wake Jangwani haukuwa rahisi. Kiungo huyo alichelewa kujiunga na kikosi na hivyo kukosa sehemu muhimu ya maandalizi ya msimu (pre-season), hali iliyomlazimu kuanza safari ya kuifikia fitness inayohitajika kwa ushindani wa kiwango cha juu.

Hata hivyo, kadiri muda unavyokwenda, dalili za kile ambacho Ngoma anaweza kukileta kwenye kikosi cha Mngqithi zimeanza kuonekana.

Pasi zinazovunja mistari

Kitu kinachomtofautisha Ngoma ni uwezo wake wa kucheza pasi zinazoweza kuvunja mistari ya ulinzi wa mpinzani.

Hii ni aina ya uwezo ambao Yanga iliwahi kuupata kupitia Aucho, ambaye aliwahi kupewa jina la “Daktari” kutokana na uwezo wake wa kucheza pasi, kutuliza mchezo na kuunganisha safu ya ulinzi na kiungo. Ngoma pia ameonyesha dalili za kuwa na uwezo huo.

Badala ya kucheza mpira wa haraka usio na mwelekeo, anaweza kusaidia timu kudhibiti tempo ya mchezo, kusogeza mpira kutoka eneo moja kwenda jingine na kutafuta nafasi ya kupenyeza mpira nyuma ya safu ya kiungo ya mpinzani.

Kwa Yanga, uwepo wa mchezaji mwenye uwezo huo unaweza kuongeza chaguo katika namna timu inavyojenga mashambulizi kutoka nyuma.

Changamoto kubwa kwake ni muda

Kwa kuwa alichelewa kujiunga na kikosi na hakushiriki kikamilifu katika maandalizi ya awali ya msimu, amekuwa akihitaji muda wa ziada kurejesha kiwango chake cha utimamu wa mwili.

Hiyo inaweza kuwa moja ya sababu zinazomfanya asitumike mara kwa mara katika michezo yenye ushindani mkubwa. Lakini mapumziko ya kalenda ya FIFA yanaweza kuwa kipindi muhimu kwake.

Kocha mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, alieleza nia ya kutumia kipindi hiki kuwaimarisha wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika pre-season.

Kwa Ngoma, hiyo inaweza kuwa fursa muhimu ya kuongeza fitness, kuelewa zaidi mfumo wa Mngqithi na kujenga muunganiko na wachezaji wenzake.

Atabiriwa makubwa Yanga

Yanga imeanza msimu kwa kiwango kizuri, lakini msimu mrefu huhitaji zaidi ya kikosi cha wachezaji 11. Hapo ndipo Ngoma anapoweza kuwa muhimu.

Iwapo ataendelea kufikia kiwango kinachohitajika kimwili, uwezo wake wa kukaba, kupokea mpira chini ya presha na kusambaza pasi zinazovunja mistari unaweza kumpa Mngqithi chaguo jingine katika eneo la kiungo.

Zaidi ya kuzuia mashambulizi ya wapinzani, kiungo wa aina hiyo anaweza kuwa na jukumu la kuanzisha mashambulizi na kudhibiti kasi ya mchezo.

Hilo ndilo eneo ambalo mashabiki wa Yanga watakuwa wakilitazama kwa karibu ligi itakaporejea. Uwepo wake akishirikiana na akina Duke Abuya bila shaka utaiongezea Yanga utulivu katika eneo hilo muhimu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
2h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’