Yanga imepania kudhihirisha 'ubabe' wake msimu ujao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jun 2018
Yanga imepania kudhihirisha 'ubabe' wake msimu ujao
Yanga ina historia ya kipekee katika soka la Tanzania. Imetwaa ubingwa wa ligi mara 27, mara 10 ikiwa kuanzia mwaka 2000.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000, Yanga ndio timu pekee iliyofanikiwa kutwaa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo ikifanya hivyo 2014/15, 2015/16 na 2016/17.

Takwimu za ubingwa kuanzia mwaka 2000

Mwaka 2000 - Mtibwa Sugar
Mwaka 2001 - Simba
Mwaka 2002 - Yanga
Mwaka 2003 - Simba
Mwaka 2004 - Simba
Mwaka 2005 - Yanga
Mwaka 2006 - Yanga
Mwaka 2007 - Simba
Mwaka 2008 - Yanga
Mwaka 2009 - Yanga
Mwaka 2010 - Simba
Mwaka 2011 - Yanga
Mwaka 2012 - Simba
Mwaka 2013 - Yanga
Mwaka 2014 - Azam FC
Mwaka 2015 - Yanga
Mwaka 2016 - Yanga
Mwaka 2017 - Yanga
Mwaka 2018 - Simba

Yanga imekuwa na kawaida ya kurejea imara msimu unaofuata kila inapokuwa imepoteza ubingwa na hiyo ndiyo sababu pekee inayoifanya timu hiyo iwe na mataji mengi kuliko timu nyingine.

Kuanzia mwaka 2000, mara ya mwisho kwa Simba kutwaa ubingwa kwa misimu miwili mfululizo ilikuwa mwaka 2003 na 2004.

Misimu mingine iliyofuata Yanga imekuwa na kawaida ya kurejesha ubingwa wake kila baada ya msimu mmoja iliyopoteza.

Baada ya misukosuko msimu uliomalizika, hakuna shaka Yanga msimu ujao itarejea imara kama ilivyo kawaida yake

Msimu ujao Yanga haitakabiliwa na ratiba ngumu kama ilivyokuwa kwenye msimu uliomalizika. Itakuwa na ratiba ya michezo ya ligi na michuano ya kombe la FA pekee.

Pia ushiriki wake katika michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi utaifanya Yanga iingie kwenye ligi msimu ujao ikiwa imeiva hasa.

Kwa sasa viongozi wa timu hiyo 'wamejifungia' wakikisuka upya kikosi chao kuhakikisha kinarejesha heshima yake msimu ujao.

Baada ya Simba kutawazwa mabingwa wa VPL msimu wa 2017/18, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema ni vyema wakafurahi sana wakati huu kwani hakuna namna watachukua ubingwa huo msimu ujao.

"Tumewaachia kwa mwaka huu wafurahi, furaha zao ni msimu huu tu, msimu ujao tutalichukua kombe letu," alisema Mkwasa

Mkwasa aliwaambia mashabiki wa Yanga wasiumizwe sana na kupoteza ubingwa na badala yake waunganishe nguvu zao kwenye kuiandaa timu kwa ajili ya msimu ujao.

Yanga itaanza maandalizi ya michezo ya kombe la Shirikisho Jumatatu ijayo, Juni 25 2018.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’