Wiki ya kazi kwa mastaa wa Yanga timu za Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Sep 2026
Wiki ya kazi kwa mastaa wa Yanga timu za Taifa

Wakati Ligi Kuu ya NBC ikisimama kwa muda kupisha kalenda ya kimataifa ya FIFA, macho yote ya wapenda soka barani Afrika sasa yanaelekezwa kwenye mbio za kuelekea AFCON 2027.

Lakini ukitaka kujua ni timu gani yenye nguvu kubwa ya ushawishi kwa sasa, usiangalie mbali, itazame Yanga. Safari hii, miamba hiyo ya Jangwani imepeleka wimbi la wachezaji 12 kwenye timu tofauti za taifa, huku nyota wake wakitarajiwa kuwa nguzo muhimu katika vikosi vyao vya kwanza. 

Kwanza kabisa, kule kwenye kikosi cha 'Taifa Stars' ya Tanzania, Yanga imetoa uti wa mgongo wa timu. Ukuta wa chuma unaoundwa na Ibrahim Bacca na nahodha Bakari Mwamnyeto utakabiliwa na kibarua kizito cha kuwazuia washambuliaji wa Guinea-Bissau mnamo Septemba 25 pale Amaan, Zanzibar, kabla ya kusafiri kwenda Casablanca kukabiliana na Madagascar.

Kwenye safu ya kiungo, Mudathir Yahya anatarajiwa kuendeleza umahiri wake huku beki wa kushoto Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' na mshambuliaji Seleman Mwalimu wakitarajiwa kuwa nguzo muhimu ya kikosi cha Stars.

Ingawa Tanzania ni mwenyeji mwenza wa fainali hizo na imeshafuzu moja kwa moja, mechi hizi ni kwa ajili ya maandalizi ya kipimo muhimu cha utayari kuelekea michuano hiyo itakayofanyika Juni 2027.

 Ukiachana na Bongo, presha kubwa itakuwa kwenye Kundi G, ambapo mashabiki wa Yanga watashuhudia "Dabi ya Jangwani" ya kipekee kabisa. Hussein Zakouane wa Comoros atakabiliana ana kwa ana na mshambuliaji hatari wa Namibia, Peter Shalulile, mnamo Septemba 29.

Hii itakuwa vita ya kusisimua kwani wachezaji hawa wanaofanya kazi pamoja kuwapa furaha Wana-Jangwani, sasa watakuwa maadui wa dakika 90 wakipigania mataifa yao.

Shalulile anabeba matumaini ya Namibia 'Brave Warriors' mchezo wao wa kwanza ukiwa dhidi ya Congo, huku Zakouane akianza kwa kuiongoza Comoros kuwatazama machoni miamba Cameroon.

Upande wa Kenya, kiungo kiraka Duke Abuya ameitwa kusaidia Harambee Stars kwenye kundi lao gumu linalojumuisha Afrika Kusini na Guinea. Wakenya wanatarajia atafanya maajabu dhidi ya Eritrea na Guinea.

Ukuta wa timu ya Taifa ya Mali utakuwa chini ya ulinzi thabiti wa golikipa nambari moja wa Yanga, Djigui Diarra. Diarra, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora, atakuwa langoni Mali ikipambana na Cape Verde na Liberia. 

Kule Zambia kiungo mshambuliaji Albert Kangwanda yeye atakuwa na kazi mbele ya Algeria katika mchezo utakaopigwa Septemba 29. Kangwanda ni mchezaji pekee aliyeitwa timu ya Taifa ya Zambia miongoni mwa wachezaji kutoka Zambia wanaocheza ligi kuu ya NBC.

Uteuzi wa wachezaji wengi kwenye timu za Taifa si tu kwamba unaleta sifa kwa klabu ya Yanga, bali ni thibitisho tosha kuwa kiwango cha soka la Tanzania kimekuwa na sasa klabu za ndani zina uwezo wa kuvutia wachezaji wa daraja la juu barani Afrika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
2h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’