Manqoba nae aenda mapumziko Afrika Kusini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2026
Manqoba nae aenda mapumziko Afrika Kusini

Kocha Mkuu wa mabingwa wa Tanzania, Yanga SC, Manqoba Mngqithi, ametumia mapumziko ya kalenda ya kimataifa ya FIFA kurejea nchini Afrika Kusini kwa mapumziko mafupi kabla ya kurejea kuendelea na majukumu yake ndani ya kikosi cha Wananchi.

Mngqithi amesafiri nyumbani wakati Ligi Kuu ya NBC ikiwa imesimama kupisha mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), huku kocha huyo akipata nafasi ya kupumzika baada ya mwanzo wa msimu wenye majukumu mbalimbali.

Kocha huyo pia amewaruhusu wachezaji wa Yanga ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa kutumia kipindi hiki kwa mapumziko kabla ya kurejea kambini kwa maandalizi ya ratiba inayofuata.

YANGA KUREJEA SEPTEMBA 28

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea kambini Septemba 28, 2026, ambapo maandalizi yataanza kuelekea mchezo mkubwa wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo utakuwa mechi za kwanza kuikabili Yanga baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA, huku timu hiyo ikitarajiwa kukabiliana na kipindi cha msongamano wa ratiba.

Baada ya kurejea kwa ligi, Yanga inakabiliwa na mfululizo wa mechi tano ndani ya siku 17, ikiwa ni wastani wa kucheza mchezo mmoja kila baada ya siku tatu hadi nne.

CAF NAYO YAWASUBIRI

Mbali na Kariakoo Dabi, ratiba hiyo inajumuisha pia michezo miwili muhimu ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya CFFA FC ya Madagascar.

Michezo hiyo itakuwa sehemu muhimu ya mipango ya Yanga katika kampeni yake ya kimataifa, huku Mngqithi na kikosi chake waakitarajiwa kutumia kipindi cha mapumziko kujiandaa kwa changamoto hizo.

Tangu alipowasili Tanzania na kuanza rasmi majukumu yake ya kuinoa Yanga, hii ni mara ya kwanza kwa Mngqithi kurejea Afrika Kusini kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Hata hivyo, mapumziko hayo hayatakuwa marefu, kwani Septemba 28 anatarajiwa kurejea pamoja na kikosi chake kuanza maandalizi ya kipindi kigumu cha msimu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
2h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’