Manqoba afichua siri ya ubora wa Maxi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2026
Manqoba afichua siri ya ubora wa Maxi

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amefichua siri ya kiwango bora kinachoonyeshwa na kiungo Maxi Nzengeli, ambaye kwa sasa amekuwa miongoni mwa nguzo muhimu katika kikosi cha Wananchi.

Maxi ameendelea kuonyesha uwezo mkubwa tangu kuanza kwa msimu huu, akiwa tayari amefunga mabao matatu katika michezo ya Ligi Kuu. Mbali na kufunga, kiungo huyo wa DR Congo amekuwa na mchango mkubwa katika utengenezaji wa mabao.

Katika mchezo dhidi ya Geita Gold, kwa mfano, Maxi alihusika katika bao la Yanga baada ya mpira wake wa kona kuwekwa kimiani na Oumar Komara.

Nyota wa mchezo mara nne

Ubora wa Maxi unaonekana pia kupitia tuzo za mchezaji bora wa mchezo. Katika michezo sita ya ligi ambayo Yanga imecheza, Maxi ameshinda tuzo ya nyota wa mchezo mara nne, idadi inayomfanya kuwa mchezaji aliyefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi hadi sasa msimu huu.

Hali hiyo imeongeza thamani yake katika kikosi cha Manqoba, huku akitumika katika eneo la kiungo na kupewa majukumu mbalimbali kulingana na mahitaji ya timu.

Manqoba: Maxi anajitambua

Katika mchezo wa kirafiki dhidi ya St George uliochezwa juzi, Manqoba alimpa Maxi jukumu la kuongoza kikosi hicho akiwa nahodha.

Uamuzi huo ulizua mjadala miongoni mwa baadhi ya mashabiki waliotamani kumuona kiungo huyo akipewa mapumziko kutokana na kutumika mfululizo katika michezo ya Yanga.

Hata hivyo, Manqoba amesisitiza kuwa Maxi ni mchezaji anayejitambua, anayeheshimu majukumu yake na ambaye huwa tayari wakati wote kuisaidia timu.

“Maxi ni mchezaji ambaye ni mshindani na wakati wowote yupo tayari kuichezea timu. Huwezi kumuona anaweka sababu zitakazomfanya akose mazoezi au jambo lolote la timu. Kwangu huyu ni muhimu sana kwenye kikosi,” amesema Manqoba.

Kocha huyo pia amewataka mashabiki wasione kama benchi la ufundi linamlazimisha Maxi kucheza bila mapumziko, akieleza kuwa mchezaji huyo anajua namna ya kuutunza mwili wake.

“Maxi atapumzika na ni mchezaji ambaye anajitunza zaidi kwa kujua kupumzika wakati ambao anatakiwa kupumzika na anayeheshimu muda wakati wote. Hivyo mashabiki wasione kama tunamuonea, ila waone ana juhudi za kutimiza majukumu yake na kusaidia timu. Hilo ndilo muhimu sana kwa sasa,” amesema Manqoba.

Kwa mwenendo wake hadi sasa, Maxi ameendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wanaobeba matumaini ya Yanga katika eneo la kiungo, huku uwezo wake wa kufunga, kutengeneza nafasi na kuchangia mabao ukimfanya kuwa sehemu muhimu ya mipango ya Manqoba msimu huu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
2h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’