Zakouane ajumuishwa timu ya Taifa Comoros

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2026
Zakouane ajumuishwa timu ya Taifa Comoros

Winga wa Yanga, Housseine Zakouani, amejumuishwa rasmi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Comoros (Coelacanths) kilichotangazwa na kocha mkuu Hubert Velud kwa ajili ya kampeni ya kufuzu AFCON 2027.

Zakouani ni miongoni mwa nyota 24 walioitwa kuitumikia nchi hiyo katika michezo miwili mikubwa ya kimataifa inayotarajiwa kupigwa mwishoni mwa mwezi huu wa Septemba.

Comoros itashuka dimbani Septemba 24 kuwakaribisha miamba wa soka barani Afrika, Cameroon, kabla ya kusafiri kuwafuata Namibia katika mchezo utakaopigwa Septemba 29.

Uteuzi wa Zakouani unakuja akiwa ameanza kuonyesha cheche zake ndani ya kikosi cha Yanga, baada ya kusajiliwa kwenye dirisha lililopita akitokea klabu ya Al-Zulfi ya Saudi Arabia.

Septemba 29 Zakouani atavaana ana kwa ana na mshambuliaji tegemeo wa Namibia na klabu ya Yanga, Peter Shalulile, katika vita ya nyota hao wa Yanga.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
2h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’