Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kusmama kwa takribani wiki tatu kupisha kalenda ya FIFA ambapo mchezo unaofuata baada ya mapumziko hayo ni Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba.
Mtanange huo utapigwa Oktoba 10 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Furaha ya Wananchi ni kuona wakati ligi ikisimama kwa kipindi hicho timu yao inatamba pale kileleni mwa msimamo wa ligi.
Yanga ndio timu yenye takwimu bora zaidi katika mechi sita, wakishinda zote huku wakifunga mabao 16 na kuruhusu mabao mawili.
Licha ya ushindi ambao Simba waliupata dhidi ya Azam Fc jana, haujawaondoa kwenye nafasi ya pili.
Yanga itangia kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo huku ikiwa kileleni...!

ADVERTISE HERE