St George tayari wamewasili nchini kuikabili Yanga mechi ya kirafiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2026
St George tayari wamewasili nchini kuikabili Yanga mechi ya kirafiki

Timu ya St George tayari imewasili nchini kuelekea mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga.

Kesho Ijumaa, Septemba 18 saa 12 jioni, timu hizo zitamenyana katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo utawahusisha wachezaji wa Yanga ambao hawakuitwa kwenye majukumu ya timu za Taifa kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2027.

Nyota wa Yanga waliojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ni mlinda lango Hussein Masalanga, mabeki Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Mohammed Hussein na Mohamed Mussa.

Pia wamo kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Seleman Mwalimu 'Gomez'. Kiungo mshambuliaji Albert Kangwanda ameitwa timu ya Taifa ya Zambia huku mshambuliaji Peter Shalulile ameitwa timu ya Taifa ya Namibia.

Aidha mlinda lango Djigui Diarra nae anatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Mali.

Mkufunzi wa Yanga Manqoba Mngqithi anatarajiwa kutumia mchezo huo kuwapa nafasi nyota wengine waliosalia yakiwa pia ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Simba.

St George inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga Srediovic Micho.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
2h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’