Yanga yasaini Mkataba wa Ujenzi wa Yanga Tower

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Sep 2026
Yanga yasaini Mkataba wa Ujenzi wa Yanga Tower

Klabu ya Yanga imeandika sura mpya katika historia yake baada ya kusaini rasmi mkataba wa ujenzi wa jengo la kisasa la kibiashara, Yanga Tower, litakalojengwa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema mradi huo ni utekelezaji wa maono ya muda mrefu ya wazee wa klabu hiyo, ambao tangu miaka ya 1960 walitamani kuwa na jengo litakalokuwa makao na chanzo cha shughuli za taasisi.

Injinia Hersi amesema juhudi za kupata eneo hilo zilihusisha hata klabu kucheza mechi za kirafiki na kutumia mapato ya milangoni kusaidia kununua ardhi hiyo. Miongoni mwa mechi hizo ilikuwa dhidi ya klabu ya Leopards ya Kenya, hatua ambayo inaendelea kuwa sehemu muhimu ya historia ya Yanga.

“Leo sisi tumebeba jukumu la kuendeleza maono hayo. Tunapoanza safari hii ya ujenzi hatujengi tu jengo, tunajenga historia, tunajenga urithi na tunajenga kwa ajili ya vizazi vijavyo,” alisema Hersi.

Mkataba wa Shilingi Bilioni 5.5

Ujenzi wa Yanga Tower utatekelezwa na Group Six International, kampuni iliyopatikana baada ya mchakato wa zabuni na tathmini ya uwezo, ubora wa kazi, gharama na muda wa utekelezaji.

Mkataba huo una thamani ya Shilingi bilioni 5.5, huku mradi ukitarajiwa kukamilika ndani ya takribani miezi 12.

Jengo hilo litakuwa na matumizi mchanganyiko, likiwa na maeneo ya biashara katika basement, ground floor na first floor, huku ghorofa ya pili hadi ya kumi zikitumika kama maghala ya kuhifadhi bidhaa.

Ghorofa ya 11 na 12 zitatengwa kwa ajili ya makazi, zikiwa na takribani units 13, wakati rooftop itakuwa eneo la kijamii litakalotumika kwa mapumziko, kahawa na chakula, mikutano pamoja na kutazama michezo.

Kwa muundo huo, Yanga Tower inalenga kuwa zaidi ya jengo la klabu, bali kituo cha biashara, makazi na shughuli za kijamii katikati ya Kariakoo.

Azania Bank Yatoa Ufadhili

Katika hatua nyingine muhimu, Azania Bank ndiyo benki itakayofadhili ujenzi wa mradi huo kwa kiasi cha Shilingi bilioni 5.5.

Mkurugenzi wa Mali na Miamala wa Azania Bank, Eugene Kimaro, amesema benki hiyo inaamini katika maono ya Yanga na iko tayari kuhakikisha fedha za mradi zinapatikana na utekelezaji unafanyika kama ulivyopangwa.

“Nimpongeze sana Injinia Hersi kwa maono yake ya kuifanya klabu hii kuwa ya mfano katika kila idara. Ndani ya miezi 12 tunatarajia kurejea hapa kwa ajili ya kuzindua jengo hili,” alisema Kimaro.

Kwa upande wake, Group Six kupitia QS Leon, imeahidi kuzingatia mambo matatu makuu katika utekelezaji wa mradi huo: thamani ya fedha, ubora wa kazi na muda.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’