Pacome awatumia ujumbe wachezaji Botswana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2026
Pacome awatumia ujumbe wachezaji Botswana

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua, amewatumia ujumbe wa hamasa wachezaji na familia nzima ya Wananchi kuelekea kuanza kwa safari ya klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pacome, ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa sasa akiendelea kuuguza jeraha la mguu, amesema moyo na mawazo yake yako pamoja na timu katika kipindi hiki muhimu.

Kupitia ujumbe wake, nyota huyo amewataka wachezaji wa Yanga kupambana hadi dakika ya mwisho, wakicheza kwa kujituma na kuhakikisha wanaibeba vyema jezi ya klabu hiyo.

β€œBahati njema kwa familia nzima ya Yanga katika safari hii mpya ya Champions League. Kwa bahati mbaya, kutokuwepo kwangu kunanifanya nisiwe pamoja nanyi uwanjani, lakini moyo na mawazo yangu yako pamoja na timu.”

Pacome ameongeza kuwa anaamini uwezo wa kikosi hicho na ataendelea kuwaunga mkono hata akiwa mbali.

β€œToeni kila kitu, piganeni hadi mwisho na ifanyieni heshima jezi yetu. Ninawaamini na nitakuwa pamoja nanyi, hata kutoka mbali,” aliandika

Yanga inaanza safari yake ya ligi ya mabingwa leo kwa mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Gaborone United utakaopigwa uwanja wa Taifa wa Botswana usiku wa leo saa 2 kwa saa za Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’