Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua, amewatumia ujumbe wa hamasa wachezaji na familia nzima ya Wananchi kuelekea kuanza kwa safari ya klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pacome, ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa sasa akiendelea kuuguza jeraha la mguu, amesema moyo na mawazo yake yako pamoja na timu katika kipindi hiki muhimu.
Kupitia ujumbe wake, nyota huyo amewataka wachezaji wa Yanga kupambana hadi dakika ya mwisho, wakicheza kwa kujituma na kuhakikisha wanaibeba vyema jezi ya klabu hiyo.
βBahati njema kwa familia nzima ya Yanga katika safari hii mpya ya Champions League. Kwa bahati mbaya, kutokuwepo kwangu kunanifanya nisiwe pamoja nanyi uwanjani, lakini moyo na mawazo yangu yako pamoja na timu.β
Pacome ameongeza kuwa anaamini uwezo wa kikosi hicho na ataendelea kuwaunga mkono hata akiwa mbali.
βToeni kila kitu, piganeni hadi mwisho na ifanyieni heshima jezi yetu. Ninawaamini na nitakuwa pamoja nanyi, hata kutoka mbali,β aliandika
Yanga inaanza safari yake ya ligi ya mabingwa leo kwa mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Gaborone United utakaopigwa uwanja wa Taifa wa Botswana usiku wa leo saa 2 kwa saa za Tanzania