FT : Fountain Gate 0-2 Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2026
FT : Fountain Gate 0-2 Yanga, NBC PL

Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi ikiichapa Fountain Gate mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Licha ya kuwa ugenini, ni Yanga iliyotawala mchezo huo na kuwaweka nyuma kwa muda mwingi Fountain Gate wakijilinda.

Wananchi walihitaji dakika 26 kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Peter Shalulile 'Shasha Man' aliyefunga kwa ustadi akiwa ndani ya eneo la hatari baada ya kupokea pasi ya kisigino kutoka kwa Stephane Aziz Ki ambaye leo ameandikisha urejeo wake kwa kutoa pasi ya bao.

Bao hilo liliipeleka Yanga mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Kipindi cha piliΒ  Wananchi waliendelea kutawala kocha Mnqoba Mngqithi akiwaingiza Mudathir Yahya na Seleman Mwalimu akiwatoa Cheick Toure na Salum Abubakar 'Sure Boy'.

Yanga ikaandikisha bao la pili kwenye dakika ya 76 Mudathir akifunga bao hilo akimalizia mpira uliokolewa na mlinda lango wa Fountain Gate Parapanda baada ya shuti la Mwalimu.

Kabla ya kuingia kwa bao hilo Aziz Ki alimanusra afunge kama shuti lake kutoka nje ya 18 lisingegonga mwamba na kurejea uwanjani.

Dakika 90 za mchezo huo zikatamatika kwa Yanga kupata ushindi wa tano mfululizo na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’