Mbivu, mbichi za wanaoachwa Yanga kujulikana karibuni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2018
Mbivu, mbichi za wanaoachwa Yanga kujulikana karibuni
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema baada ya kukamilisha zoezi la kuhuisha mikataba ya wachezaji iliyomalizika pia kukamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji wapya, wataweka hadharani orodha ya wachezaji wanaoachwa.

Msimu huu Yanga inaendesha usajili wake kwa usiri mkubwa, uamuzi unaoelezwa kufikiwa kuepuka hujuma kutoka kwa timu pinzani.

Mkwasa amesema kwa sasa bado wanaendelea na mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika, wakitarajia kukamilisha zoezi hilo kabla ya kikosi cha Yanga kuanza mazoezi Jumatatu ijayo, Juni 25.

Moja ya sababu iliyotolewa na uongozi wa Yanga ilipojitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame ni kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao hawana mikataba.

Taarifa iliyowasilishwa na uongozi wa Yanga kwa Kamati Maalum ya mpito inayoongozwa na Abbas Tarimba, ilieleza kuwa na wachezaji saba tu wenye mikataba.

Wakati huo huo, Mkwasa amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kutotishika na usajili unaofanywa na baadhi ya timu kwa kuwa kila timu inasajili kufuatana na mahitaji yake.

Kati ya timu vigogo nchini, Yanga ndio timu pekee ambayo haijaweka wazi majina ya wachezaji iliyowasajili huku idadi kubwa ya wachezaji nyota waliotamba katika vilabu mbalimbali msimu uliomalizika wakitua katika timu za Singida United, Simba na Azam FC.

Jana klabu ya Singida United imetangaza kumsajili mshambuliaji wa Prisons, Eliuter Mpepo ambaye anaongeza idadi ya wachezaji nyota waliosajiliwa na wapinzani hao wa Yanga.

Wachezaji wengine waliotamba msimu uliomalizika na tayari wametua kwa timu pinzani ni pamoja na Habibu Kiyombo (Singida United), Tiber John (Singida United), Mohammed Rashid (Simba), Adam Salamba (Simba) na Marcel Kaheza (Simba).

Wengine ni Kazungu Mashauri (Singida United), Mudathir Yahya (Azam FC), Ditram Nchimbi (Azam FC) na Tafadzwa Kutinyu (Azam FC).

"Msimu huu tumeamua kufanya usajili kwa umakini zaidi. hatutaki kusajili wachezaji hovyohovyo halafu baadae tukaja kujilaumu," amesema Mkwasa.

"Ni kweli baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na timu nyingine sisi tulianza kufanya nao mazungumzo, lakini wenzetu wakawahi kuwasajili, lakini kwa utaratibu tunaotumia sasa, jambo hilo halitatokea tena."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
10h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’