Aziz Ki kuanza na Fountain Gate leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2026
Aziz Ki kuanza na Fountain Gate leo?

Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji ambao jana walishiriki kikamilifu maandalizi ya mwisho ya Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Tangu akamilishe usajili wake kurejea Yanga, Aziz Ki amekuwa kwenye program maalum ya mazoezi kuimarisha utimamu wake wa mwili 'fitness' kabla ya kuanza rasmi majukumu yake.

Hata hivyo kitendo cha kujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilichotua Arusha kuikabili Fountain Gate ni wazi huenda kocha Manqoba Mngqithi ana mpango wa kumtumia kwenye mchezo huo.

Ikumbukwe baada ya mchezo huo, Yanga itaelekea Botswana kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United.

Manqoba atamuhitaji Aziz Ki kwenye michuano hiyo mikubwa ambayo Yanga imeweka malengo ya kufanya vizuri zaidi msimu huu.

Kuna uwezekano mkubwa Aziz Ki leo akaonekana kwenye kikosi cha Wananchi kwa mara ya kwanza tangu urejeo wake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’