Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako mkoani Arusha kumenyana na Fountain Gate katika mchezo wa mapema utakaopigwa saa 10 jioni.
Yanga inayoongoza ligi, imetua Arusha ikiwa na mkakati wa kuendeleza rekodi nzuri ya ushindi wa asilimia 100 msimu huu.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari jana, Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alikiri kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi lakini anaamin vijana wake watafanya kiile walichoandaa kwenye uwanja wa mazoezi na kuibuka na ushindi.
Mchezo huo Yanga itautumia kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United utakaopigwa mwishoni mwa wiki huko Botswana.
Yanga ilikamilisha maandalizi yake ya mwisho jana ari na morali ya timu ikiwa juu kuelekea mtanange huo ambao ushindi kwa Wananchi unaweza kuwaimarisha kwenye nafasi yao juu ya msimamo.