Pamba Jiji watachagua wafungwe na nani leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2026
Pamba Jiji watachagua wafungwe na nani leo

Mashabiki wa Yanga wanahesabu masaa kabla ya kuelekea uwanja wa KMC Complex kuishuhudia timu yao ikichuana na Pamba Jiji katika mchezo wa raundi ya nne wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa saa 3:00 usiku.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya mechi tatu zilizopita, ambazo wamefunga mabao 11 na wakikusanya alama 9 na kuruhusu mawili pekee, huku safu ya wafumania nyavu ikiongozwa na wakali kama Peter Shalulile, Maxi Nzengeli, Albert Kangwanda na beki wa kushoto Chadrack Boka ambaye msimu huu ni kama amezaliwa upya.

Macho ya mashabiki leo yatakuwa kwa mshambuliaji mpya Seleman Mwalimu, ambaye anaweza kupewa nafasi ya kuanza kuitumikia Yanga baada ya taratibu za usajili wake kukamilika.

Unaweza kusema Pamba Jiji watakuwa na kazi ya ziada na watapaswa kuwa kwenye ubora mkubwa kuepuka kipigo kutoka kwa mabingwa hao watetezi.

Wakulima hao wa Pamba watangia dimba la KMC Complex wakifahamu wanahitaji kuzuia mashambulizi ya Yanga ambayo yatakuwa yakitoka kila upande.

Upande wa kushoto watarajie kukutana na Boka na Hussein Zakouani wakiwa miongoni mwa wachezaji waliohusika kwenye mabao mengi mpaka sasa.

Lakini upande wa kulia yupo Yao Kouassi 'Jeshi' na Kangwanda ambaye yeye hupendelea kuingia ndani na kumuachia Yao kushambulia upande huo.

Yanga hii yeyote anakufunga! kwani kwenye mchezo uliopita tumemshuhudia beki Ibrahim Bacca akifunga moja ya mabao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Mipira ya kutenga nayo imekuwa silaha kubwa kwa Yanga msimu huu, kwa Yanga hii kona na mipira ya adhabu karibu na lango ni sawa na pigo la penalti! 

Yanga ina mtaalam wa mipira hiyo Kagisho Dikgacoi ambaye mapema tu kazi yake imeanza kuonekana kwa Yanga kutumia vyema mipira hiyo kufunga mabao.

Leo Yanga wanahitaji ushindi ili kurejea kileleni mwa msimamo, huku Pamba Jiji wakitarajiwa kutumia nidhamu ya ulinzi kujinusuru na kipigo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’