Mzize bado kidogo tu, tutamuona uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2026
Mzize bado kidogo tu, tutamuona uwanjani

Mashabiki wa Yanga SC wanaweza kuanza kuhesabu siku za kumuona tena mshambuliaji Clement Mzize akirejea uwanjani baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na jeraha la goti.

Mzize amekuwa nje ya uwanja kwa karibu msimu mzima akiuguza jeraha hilo. Hata hivyo, kwa sasa nyota huyo amepona na ameanza kufanya mazoezi pamoja na timu, hatua inayotoa matumaini makubwa ya kurejea kwake katika kikosi.

Mzize na beki Dickson Job ndio wachezaji pekee wa Yanga ambao wamekuwa nje ya uwanja tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na majeraha.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema Mzize ameendelea kuimarika na huenda akarejea uwanjani mapema zaidi ya ilivyotarajiwa.

Kwa mujibu wa Kamwe, taarifa ya awali ilionyesha kuwa Mzize na Job walitarajiwa kurejea uwanjani mwanzoni mwa Oktoba. Hata hivyo, maendeleo mazuri wanayoendelea kuyaonyesha katika uwanja wa mazooezi yanaweza kufanya kurejea kwao kuwa mapema.

Mzize, ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji wanaoaminika katika kikosi cha Yanga, anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji mara atakapokuwa tayari kurejea kwenye ushindani wa mechi rasmi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’