Yanga imefanikiwa Hapa: Siri ya Injinia Hersi kuhusu uaminifu wa wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2026
Yanga imefanikiwa Hapa: Siri ya Injinia Hersi kuhusu uaminifu wa wachezaji Yanga

Katika ulimwengu wa soka la kisasa, usajili wa wachezaji umekuwa ukiendeshwa zaidi na maslahi ya kifedha kuliko kitu kingine chochote. Hata hivyo, Klabu ya soka ya Yanga  inaonekana kugundua fomula ya kipekee inayowatofautisha na klabu nyingine nchini na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Siri hii kubwa imewekwa wazi na Rais wa Klabu hiyo, Injinia Hersi Said, hivi karibuni wakati wa hafla ya kumtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, iliyofanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Wachezaji ni Wanachama: Zaidi ya Mkataba wa Kazi

Injinia Hersi alifichua kuwa mchakato wa kumrejesha Aziz Ki ulichagizwa na uhusiano wa kimfumo uliopo kati ya mchezaji na klabu.

Alieleza kuwa wachezaji wote wanaoitumikia Yanga wanajengewa mazingira ya kuwa Wanachama hai wa klabu hiyo. "Wachezaji wetu ni Wanachama wa Yanga," alisema Hersi, akisisitiza kuwa mfumo huu unawafanya wachezaji kuiona timu hiyo kama familia yao ya kudumu.

Ndiyo maana inakuwa rahisi kwao kurejea au kubaki klabuni hapo hata pale wanapopata ofa nono kwingineko, kwa sababu mapenzi yao kwa nembo ya klabu yanavuka mipaka ya mkataba wa fedha.

Kauli ya Injinia Hersi haikuishia kwenye sifa tu, bali iliwagusa watani zao wa jadi, Simba SC. Hii inakuja kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo Yanga ilifanikiwa kumsajili mshambuliaji Selemani Mwalimu, ambaye aliripotiwa "kuchomolewa" moja kwa moja kutoka kwenye kambi ya Simba visiwani Zanzibar.

Hersi alisema kwa kujiamini kuwa jambo kama hilo haliwezi kutokea Avic Town ilipo kambi ya Yanga Sc.

"Nawaruhusu nendeni pale Avic Town kajaribuni 'kumchomoa' mchezaji yeyote muone kama itawezekana. Wachezaji wetu ni Wanachama wa Yanga," alitamba Hersi

Yanga imefanikiwa Hapa

Hapa ndipo Yanga ilipofanya mapinduzi makubwa ya kiutawala (Psychological Management). Kwa kuwabadilisha wachezaji kutoka kuwa "waajiriwa tu" na kuwa "wanachama na wenye hisa wa klabu kihisia".

Yanga inatengeneza ngome isiyopenyeka kwa urahisi na mawakala au timu pinzani.Mchezaji anayejitambua kama mwanachama anakuwa tayari kupambana kwa jasho na damu uwanjani, na analinda siri pamoja na hadhi ya klabu hata anapokuwa nje ya uwanja.

Huu ni ukomavu wa klabu unaoonyesha kwa nini Yanga inaendelea kutawala soka la ndani na kufanya vizuri kimataifa.

Misimu mitano mfululizo Yanga imetwaa taji la ligi kuu, licha ya changamoto nyingi msimu ulopita, wachezaji walipambana kwa jasho na damu kuhakikisha wanatwaa ubingwa.

Msimu huu wananchi wamerejea tena kwa nguvu kubwa lengo likuwa kuendeleza ubabe wa ndani na kufanya vyema zaidi kwenye ligi ya mabijngwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’