Manqoba amkaribisha Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2026
Manqoba amkaribisha Aziz Ki

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi ameeleza kufurahishwa na usajili wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki anayerejea Yanga kwa mara ya pili.

Juzi Yanga ilitambulisha usajili wa Aziz Ki aliyerejea kutoka klabu ya Al Ittihad ambayo aliitumikia kwa miezi sita tu tangu alipojiunga nayo akitokea Wydad CA.

Manqoba amesema Aziz Ki ni aina ya mchezaji ambaye kila kocha anatamani kuwa nae kutokana na kipaji alichonacho na uwezo wake kuisaidia timu hasa katika nyakati ngumu.

"Kiukweli nina furaha sana kwasababu nilikuwa nasubiri kwa hamu usajili huu na namshukuru Rais wa timu, Bodi na kila mmoja aliyehusika kuhakikisha hili linatokea."

"Sisi ni timu ambayo ina malengo makubwa sana, tunataka kushinda makombe kwa kadiri tuwezavyo."

"Hivyo Tunahitaji wachezaji na si hivyo tu bali wachezaji ambao wanaweza kuweka utofauti pale tunapohitaji kwahiyo Aziz anaenda kuongeza thamani kubwa kwenye kikosi chetu."

"Niliongea naye hata huko Afrika Kusini baada ya kuonyesha kiwango kizuri sana dhidi ya Sundowns. Kwenye timu yangu, anapaswa kuwa tayari kukimbia na kupambana kama wachezaji wengine wote," alisema Manqoba.

Aziz Ki leo anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake kwenye maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union utakaopigwa August 20 uwanja wa KMC Complex.

Aziz Ki amechukua nafasi ya Allan Okello ambaye amejiunga na klabu ya AS FAR Rabat ya Morocco akiungana na kocha wa zamani wa Yanga Pedro Goncalves

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
46m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’