Kila la 'Star Boy' Allain Okello

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Aug 2026
Kila la 'Star Boy' Allain Okello

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya NBC nchini, Yanga SC, wamethibitisha kumuuza kiungo wao mshambuliaji raia wa Uganda, Allan Okello, kwenda klabu ya AS FAR Rabat ya Morocco kwa dau linalokadiriwa kufikia Tsh Bilioni 3.

Hatua hiyo imekuja sambamba na klabu hiyo kumtambulisha rasmi kiungo wao wa zamani na kipenzi cha mashabiki, Stephane Aziz Ki, ambaye anarejea kuchukua nafasi hiyo.

Yanga iliridhia ofa hiyo kutoka kwa miamba hiyo ya Morocco baada ya Okello kuonyesha msimu mzuri uliopita, akifunga mabao 14 na kuwa mchezaji tegemeo.

AS FAR imeshinda vita dhidi ya mahasimu wao Wydad Casablanca, ambao pia walikuwa wakipambana kupata saini ya fundi huyo wa mguu wa kushoto. Okello ameungana na Pedro Goncalves aliyempokea Yanga mwezi Januari.

Okello tayari ameshaagana na wachezaji wenzake na anatarajiwa kusafiri kuelekea Rabat kwa ajili ya vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Ili kuziba pengo hilo bila kuathiri nguvu ya kikosi hicho, uongozi wa Yanga chini ya Rais, Injinia Hersi Said, umefanya umafia wa usajili kwa kumrejesha Stephane Aziz Ki kutoka Al-Ittihad Tripoli ya Libya.

Kiungo huyo raia wa Burkina Faso, ambaye alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 kwa kufunga mabao 21, amerejea kikosini hapo baada ya Yanga kununua mkataba wake huko Libya.

Aziz Ki alitambulishwa jana katika tukio la aina yake lililofanyika uwanja wa KMC Complex ambapo uwanja huo ulifurika Wananchi 'Full House'.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alimkaribisha Aziz Ki Jangwani kwa mara nyingine huku akimtakia kila la kheri Okello katika klabu yake mpya.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’