Mashabiki wa Yanga Lindi wampagawisha Manqoba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2026
Mashabiki wa Yanga Lindi wampagawisha Manqoba

Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi ameeleza kufurahishwa na mamia ya mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo mkoani Lindi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc.

Yanga iliwasili Ruangwa jana tayari kwa mtanange huo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi, August 15 kwenye uwanja wa Majaliwa.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Manqoba alisema mashabiki wameendelea kuwa sehemu muhimu ya hamasa ya kikosi chake akiamini kesho watajitokeza kwa wingi uwanja wa Majaliwa.

Aidha, licha ya kikosi chake kutopata muda wa kutosha wa maandalizi wakitoka Zanzibar kuchuana na Simba mchezo wa Ngao ya Jamii ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0, Manqoba alisema anaamini katika ubora wa wachezaji wake na matarajio yake wataendeleza mwanzo wao mzuri.

"Hatujapata muda mrefu wa kujiandaa dhidi ya Namungo lakini kwa namna tulivyojipanga tangu mchezo wa Derby naamini tutakuwa kwenye mfumo wetu ule ule na Nina amini tutapata Matokeo mazuri”

“Nimefurahi sana kuwaona Mashabiki wetu hapa Lindi, Nina amini kila siku kuwa wao ndio wachezaji wetu wa 12 uwanjani, kwakweli wanatusaidia sana kucheza kwa morali na nguvu tunapokuwa Uwanjani, Natamani kuwaona tena Kesho kwenye mechi yetu dhidi ya Namungo” 

“Ninaamini Namungo watakuja kwa kujiamini na kujihami kwa wakati huo huo, najua wana kocha mzuri sana na namjua tangu akifundisha timu ua Taifa, Hivyo nasisi tutatumia Ubora wetu na tutatengeneza nafasi zetu ili kushinda mechi,” alisema Manqoba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’