Ni leo; Yanga vs Simba, Ngao ya Jamii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Aug 2026
Ni leo; Yanga vs Simba, Ngao ya Jamii

Ni siku kubwa kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga kwani mwanzo wa msimu wa mashindano 2026/27 unafunguliwa leo visiwani Zanzibar.

Ni mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha mabingwa wa msimu uliopita ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga dhidi ya mabingwa wa kombe la CRDB klabu ya Simba.

Mchezo wa Kariakoo Derby utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex saa 2:30 usiku.

Baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi, mchezo huo utakuwa kipimo cha kwanza kwa kocha Manqoba Mngqithi na benchi lake kuona kama atawapeleka Wananchi nchi ya ahadi?

Yanga imefanya uwekezaji mkubwa kwenye dirisha hili wakisajili wachezaji wenye 'profile' kubwa kama Peter Shalulile ambaye wamemsajili kutoka klabu ya Mamelodi Sundowns.

Ni usajili uliolenga kufanya makubwa zaidi msimu huu kwenye mashindano ya ndani na ligi ya mabingwa barani Afrika.

Hautakuwa mchezo mwepesi kwani wanakutana na Simba ambayo haina mabadiliko makubwa wakiwa na benchi lao la ufundi lile lile lililomaliza nalo msimu uliopita.

Hakuna shaka kuwa Simba wameimarika sana na haishangazi msimu uliopita waliweza kuwapa ushindani Yanga kwani katika mechi nne walizokutana, kila timu ilishinda mechi moja huku wakitoka sare mechi mbili.

Hata hivyo wakati huu wanakutana na Yanga iliyofanyiwa maboresho makubwa kwenye baadhi ya maeneo hasa safu ya ushambuliaji.

Yanga ndio mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii na leo watashuka dimba la New Amaan Compex wakiwa na dhamira moja tu, kutetea Ngao hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’