Mshambuliaji mpya wa Yanga Suleiman Mwalimu amewasili visiwani Zanzibar kuungana na wachezaji wenzake tayari kwa maandalizi ya mwisho jioni ya leo kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa New Amaan Complex visiwani humo.
Mwalimu anawasili Zanzibar kwa mara ya pili katika kipindi cha siku moja na nusu lakini safari hii akiwa ndani ya uzi wa Yanga.
Jana jioni aliwasili visiwani humo na kufanya mazoezi na klabu ya Simba lakini leo atafanya mazoezi na klabu ya Yanga na pengine kesho akapata nafasi ya kuwakabili waajiri wake wa zamani klabu ya Simba.
Yanga ilimsajili Mwalimu usiku wa kuamkia leo wakimchomoa kutoka kwenye kambi ya Simba na kumsainisha mkataba saa 10 Alfajiri.
Ametua Zanzibar akiongozana na Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ali Kamwe wakipokelewa na Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji

