Gor Mahia kushiriki michuano ya Kagame ni faida kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2018
Gor Mahia kushiriki michuano ya Kagame ni faida kwa Yanga
Baada ya kujitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame inayoanza nchini Juni 28, 2018, Yanga imeipa mtihani mkubwa Gor Mahia inayoshiriki michuano hiyo.

Moja ya sababu iliyopelekea Yanga kujitoa kwenye michuano hiyo ni ukaribu wa mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya mabingwa hao wa Kenya utakaopigwa Julai 18 jijini Nairobi, Kenya.

Kushiriki kwa Gor Mahia kwenye michuano hiyo kutaipa Yanga nafasi ya kuisoma kikamilifu na pengine ikaweza kutumia madhaifu yake kupata matokeo nchini Kenya.

Kama Gor Mahia itaweza kutinga mpaka hatua ya fainali ya michuano hiyo, basi itakuwa Dar hadi Julai 13 siku tano kabla ya mchezo dhidi ya Yanga huko Kenya.

Gor Mahia ilionyesha kandanda safi kwenye michuano ya SPortPesa Super Cup iliyomaliza karibuni nchini Kenya ambapo timu hiyo ilitwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfulilizo.

Yanga imedhamiria kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Kutimiza adhma hiyo, lazima ihakikishe inapata matokeo kwenye michezo miwili dhidi ya Gor Mahia na ule wa nyumbani dhidi ya USM Alger utakaopigwa August 19.

Mchezo wa mwisho utakuwa dhidi ya Rayon SPorts, August 28
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’