Mwijage anaichukua heshima yake kwa nguvu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Aug 2026
Mwijage anaichukua heshima yake kwa nguvu

Kuna hii kasumba ya mashabiki kutothamini usajili wa wachezaji wa ndani. Ni jambo ambalo limekuwa likiwaumiza sana wachezaji wa ndani hasa wanapotambulishwa kwenye hizi timu kubwa nchini Yanga na Simba, hukumbana na maneno ya kejeli na kukatishwa tamaa.

Yaani mashabiki wamezoea mchezaji mzuri ni yule anayesajiliwa kutoka nje ya nchi, hawa wa ndani hawapewi heshima kwa ukubwa wanaostahili ingawa pia sio kwa wachezaji wote.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikumbana na 'sekeseke' hilo ni kiungo mshambuliaji Erick Mwijage ambaye Yanga imemsajiili kwenye dirisha hili akitokea klabu ya KMC.

Ni usajili ambao ukisoma maoni ya wengi mitandaoni wakati anatambulishwa, hawakumkubali kwa kuwa amesajiliwa kutoka klabu ya KMC ambayo imeshuka daraja.

Lakini kile alichoonyesha jana kwenye mchezo wa Yanga Day dhidi ya Aigle Du Congo kinaweza kuwa kimewafunga midomo wengi waliokejeli usajili wake.

Mwijage alikuwa miongoni mwa wachezaji waliong'ara kwenye dakika 45 aizotumika katika kipindi cha kwanza.

Ni miongoni mwa wachezaji walioeleweka mapema na benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Manqoba Mngqithi na pengine huenda akawa na nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha kocha huyo raia wa Afrika Kusini.

Uwezo wake wa kutumika winga nafasi zote pembeni na hata kiungo mshambuliaji namba 10, unamfanya kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Manqoba.

Kwa wale waliomfuatilia Mwijage kwenye mchezo dhidi ya Aigles Du Congo watakubaliana ni usajili makini ambao Rais wa Yanga Injinia Hersi Said anastahili pongezi.

Hersi ameendeleza msimamo wake wa kuwapa nafasi wachezaji wazawa kwenye kikosi cha Yanga licha ya ukosoaji mkali kutoka kwa baadhi ya mashabiki na hata wachambuzi.

Yawezekana kuna ukweli baadhi ya wachezaji hawafikii matarajio lakini wengine wanapoaminiwa wanafanya vyema. Mwijage anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji ambao watarejesha imani iliyoonyeshwa mapema kwake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’