Yanga Day imehitimishwa uwanja wa Uhuru kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki Yanga ikipoteza mbele ya Les Aigles Du Congo kwa mabao 2-1.
Ulikuwa mchezo uliokuwa na ushindani mkali Yanga wakitangulia kufunga kupitia kwa Peter Shalulile kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Hata hivyo Wacongomani walitumia vyema makosa ya nyota wa Yanga kupoteza mipira katika maeneo ya hatari Talasy Tonny akifunga mabao yote mawili.
Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi alitumia mchezo huo kuwapa nafasi wachezaji wengi akitumia vikosi viwili kila kipindi akitumia timu tofauti.
Aigles Du Congo wamekuwa na mchezo mzuri pia, ikiwa ni timu inayoonyesha imejipanga kufanya vyema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msiimu huu wakianza na APR hattua ya awali.