Mshambuliaji wa Yanga Peter Shalulile amefichua kuwa kwa muda amekuwa akifuatilia Tamasha la Wiki ya Wananchi sasa akipata fursa ya kuwa sehemu ya Tamasha hilo.
Shalulile amewaalika mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili kufungua msimu mpya pamoja.
"Wananchi tuonane siku ya Jumapili, nimefuatilia Tamasha hili kwa muda mrefu, njooni kwa wingi tufurahi pamoja," alisema Shalulile.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns, ni miongoni mwa wachezaji wapya ambao kwa mara ya kwanza siku ya Jumapili wanakwenda kushuhudia 'full-house' ya Wananchi wakiukaribisha msimu mpya.
Kwa miaka kadhaa sasa wiki ya Mwananchi limekuwa tukio lenye hadhi kubwa kwa wachezaji kupitia tukio hilo wachezaji wanafahamu ukubwa wa klabu wanayoitumikia na wajibu wao katika kuipambania na kuhakikisha wanashinda mataji.