Yanga kutambulisha mchezaji Bukombe Stadium

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Aug 2026
Yanga kutambulisha mchezaji Bukombe Stadium

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amedokeza mpango wa timu hiyo kumtambulisha mchezaji mpya kwenye uwanja wa Bukombe.

Kamwe amesema mchezaji huyo amejumuishwa kwenye kikosi kilichoondoka jijini Dar es salaam mapema leo kuelekea Ushirombo kwenye hafla ya ufunguzi wa uwanja wa Bukombe.

"Leo tuna matukio makubwa mawili, tukio la kwanza ni uzinduzi wa wiki ya Mwananchi halafu tukio la pili ni kushiriki uzinduzi wa uwanja wa Bukombe"

"Kwa hamasa tunayoiona Wanayanga wakiitikia kwelikweli niwaambie tu leo tumewaletea zawadi ya kumtambulisha mchezaji mwingine wa Yanga tukiwa ndani ya uwanja wa Bukombe," alisema Kamwe

Aidha, msemaji huyo wa mabingwa wa nchi pia akafichua kuwa baada ya utambulisho huo bado hawajamaliza kwani kuna mchezaji mwingine atatambulishwa katika siku chache zijazo.

"Leo tunatambulisha mmoja halafu kuna mwingine ambaye tukija kumtambulisha watu watatafutana. Huko aliko saa izi watu wanafanya nae mazoezi wanaamini ni wa kwao," alitamba Kamwe.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’