Mshambuliaji mpya wa Yanga, Peter Shalulile, anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo kuanza rasmi safari yake ya kulitumikia kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili, Shalulile atatambulishwa rasmi kwa mashabiki na vyombo vya habari leo saa 5:00 usiku, ambapo pia atasaini mkataba wake mbele ya waandishi wa habari katika hafla maalumu iliyoandaliwa na klabu hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa kutoka Namibia anajiunga na Yanga akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa kwa kipindi cha misimu sita.
Katika kipindi chake akiwa Sundowns, Shalulile aliweka rekodi ya kuvutia kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Akiwa na jezi ya Sundowns, alifunga mabao 130 kwenye mechi za ligi, huku akiongeza mabao 20 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Mashabiki wa Yanga sasa wanasubiri kwa hamu kumuona mshambuliaji huyo akianza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka nchini Tanzania, huku matumaini makubwa yakiwa ni kuona akiendelea na makali yake ya kufumania nyavu.
