Bajeti ya Yanga 2026/27 yapanda hadi Sh Bilioni 36

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2026
Bajeti ya Yanga 2026/27 yapanda hadi Sh Bilioni 36

Klabu ya Yanga imewasilisha makadirio ya bajeti ya msimu wa mashindano wa 2026/2027 yenye thamani ya Sh36.013 bilioni, ikiwa ni moja ya bajeti kubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Bajeti hiyo imewasilishwa leo na Mkurugenzi wa Fedha wa Yanga, Justina Ernest, wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi unaoendelea katika ukumbi wa The Super Dome.

Kwa mujibu wa makadirio hayo, sehemu kubwa ya matumizi itaelekezwa katika kuboresha kikosi na kuimarisha uendeshaji wa klabu. Kiasi cha Sh13.1 bilioni kimetengwa kwa ajili ya mishahara na marupurupu ya watumishi, huku Sh8.7 bilioni zikielekezwa kwenye usajili wa wachezaji wapya kwa lengo la kuijenga timu yenye ushindani mkubwa katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Aidha, bajeti hiyo pia imezingatia gharama za maandalizi ya mechi, kambi za timu, usafiri na shughuli nyingine muhimu za uendeshaji wa msimu mpya.

Kwa upande wa mapato, Yanga inatarajia kukusanya jumla ya Sh20.69 bilioni kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato, huku ikilenga kuendelea kuimarisha uwezo wake wa kifedha na ushindani.

Kwa msimu wa 2025/2026, klabu ilikusanya jumla ya TSh 29.36 bilioni. Matumizi ya klabu yalifikia TSh 29.34 bilioni, ambapo sehemu kubwa ilielekezwa kwenye mishahara na marupurupu ya watumishi, usajili na uhamisho wa wachezaji, maandalizi ya mechi, usafiri, chakula na malazi.

Baada ya matumizi hayo, klabu ilibaki na bakaa ya TSh 17.5 milioni.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’