Ngoma atambulishwa Yanga, namba sita ya boli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
2 Aug 2026
Ngoma atambulishwa Yanga, namba sita ya boli

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ametambulisha usajili wa kiungo mkabaji Fred Ngoma aliyesajiliwa kutoka klabu ya Olympic Club de Safi ya Morocco.

Ngoma anatua Yanga kuimarisha safu ya kiungo cha ukabaji, eneo ambalo limekuwana changamoto tangu aondoke Khalid Aucho

Ngoma ni kiungo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Congo-Brazzaville, msimu uliopita alikuwa silaha muhimu ya Olympique Club de Safi (OC Safi) inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro). Alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichocheza nusu fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC).

Ngoma, aliyezaliwa Novemba 24, 1997 huko Pointe-Noire, ana wasifu mkubwa na uzoefu wa kutosha katika soka la Afrika. Alianzia soka la ushindani nchini mwao akizichezea klabu za CSMD Diables Noirs, AC Léopards, na CS La Mancha, kabla ya kung'ara zaidi na AS Otôho kati ya mwaka 2018 na 2021. Akiwa na Otôho, alicheza michuano ya kimataifa ya CAF na kuitwa Timu ya Taifa ya Congo-Brazzaville.

Mbali na nyumbani kwao, kiungo huyo ana uzoefu wa miaka mingi katika soka la Kaskazini mwa Afrika. Alicheza nchini Tunisia akiwa na CA Bizertin (2021–2023), kisha akatimkia Libya kuziwakilisha Al-Ittihad Tripoli na Al-Akhdar.

Ni rasmi sasa Ngoma ni Mwananchiii...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →