Pre-season ya Yanga imeendelea kushika kazi Avic Town kocha Manqoba Mngqithi akiendelea kuziandaa silaha zake kwa ajili ya mikiki mikiki ya mashindano 2026/27.
Kuna utofauti mkubwa wa aina ya mazoezi ambayo wachezaji wanafanya chini ya benchi la ufundi la Manqoba. Hatua hiyo inadhihirisha kwa nini mabosi wa Yanga msimu huu wamewekeza kuwa na benchi bora la ufundi lenye uzoefu mkubwa.
Kwa aina ya mazoezi yanayofanyika huko Avic Town, ni salamu kwa wapinzani kuwa msimu ujao kazi itakuwa ngumu zaidi kupata chochote mbele ya mabingwa hao wa kihistoria.
Yanga inajiandaa ikilenga zaidi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL), yaani Wananchi wanajiandaa kwenda kupambania ubingwa wa Afrika!







ADVERTISE HERE