Jana Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alithibitisha kuwa nahodha wa timu hiyo Bakari Nondo Mwamnyeto ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
Mwamnyeto tayari alishaonekana viunga vya Avic Town akiendelea na maandalizi ya msimu mpya, ari na morali yake ikiwa juu.
Licha ya changamoto za ukosoaji mkali aliokumbana nao mwishoni mwa msimu uliopita, Yanga imeendelea kumuamini nahodha huyo ambaye anaelekea kuingia kwenye historia ya kunyanyua makombe mengi akiwa nahodha wa Yanga.
Mkataba wa miaka miwili aliongeza utamfanya adumu na Wananchi hadi mwaka 2028 na kuwa mchezaji mwandamizi zaidi kwenye kikosi cha sasa cha Yanga.
Yanga imeendelea kuwaamini mabeki wazawa kwenye safu yake ya ulinzi kwani msimu ujao mabeki wote wa kati ni Watanzania.
Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Mohammed Mussa aliyetua katika dirisha hili akitokea klabu ya Mashujaa Fc.