Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa saini namba sita ndio usajili mkubwa ambao Yanga wamefanya katika dirisha hili.
Aidha Kamwe amefuta tetesi zinazoihusisha Yanga na kiungo Morice Chukwu akisisitiza kuwa mchezaji waliyemsajili sio yeye.
“Saini namba sita ndiyo usajili mkubwa tulioufanya msimu huu. Tayari tumekamilisha kila kitu, kilichobaki ni siku ya utambulisho. Wanaomtaja Morice Chukwu nawaomba waondoe hofu siye tunayemzungumzia. Usajili wetu tayari umekamilika."
“Usajili tuliofanya msimu huu unaonyesha kiwango tulichojiwekea. Tumekusudia kufanya jambo kubwa na msimu huu hatukuja kutania,” alitamba Kamwe.
Kamwe amebainisha kuwa mdhamini wa Yanga, GSM kwenye dirisha hili ametumia zaidi ya Tsh Bilioni 15 kwa ajili ya kukamilisha na kuwashusha ma wata pleya Jangwani.
“Bajeti ya usajili msimu huu Rais wetu Eng. Hersi alimuita Mfadhili wetu GSM kumuuliza msimu huu tunafanyaje kusajili wachezaji GSM akamjibu kuwa tafuta wachezaji pesa nitatoa”
"Ghalib Said Mohamed ameweka bajeti ya Bilioni 15 kusajili tu wachezaji na kuna mchezaji mmoja juzi alizungumza na GSM alimtaka ila alirukaruka lakini tulitaka kumleta Yanga sc kwa jeuri ya hela aliyoweka mfadhili wetu,” alibainisha Kamwe